Ngoma ya Malinzi bado mbichi arudi selo



Hali ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana Jumatatu ilionekana kuwa ya huzuni kubwa baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri, kuahirisha kesi na kuwanyima dhamana watuhumiwa wa TFF ambao ni Rais Jamal Malinzi, Katibu Mkuu, Celestine Mwesigwa na Nsiende Mwanga ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha.
Kwa mara ya kwanza, Malinzi na wenzake walipandishwa kizimbani Juni 29 ambapo alisomewa mashitaka 28 huku watendaji hao wengine wakisomewa mashitaka matatu kila mmoja.
Mashitaka yote hayo yalihusu tuhuma za kugushi nyaraka na kutakatisha fedha na sasa kesi hiyo itasomwa Julai 17 ambapo watuhumiwa walirejeshwa rumande.
Malinzi na wenzake walifikishwa mahakamani hapo wakiwa ndani ya gari la Jeshi la Magereza pamoja na watuhumiwa wa kesi nyingine kutoka gereza la Keko.
Hakimu Mashauri alianza kwa kusoma taarifa za pande zote mbili, upande wa Mawakili wa Jamhuri na Mawakili wa Watuhumiwa wanaoongozwa na Mwanasheria wa kujitegemea Jerome Msemwa.
Alisema kuwa walalamikaji waliitaka Mahakama itoe amri kwa Jamhuri kufanya haraka juu ya upelelezi na kwamba hawakuona sababu ya watuhumiwa kufikishwa mahakamani wakati upelelezi haujakamilika.
Mashauri alikubaliana na maombi ya mawakili wa Jamhuri kwamba upelelezi bado haujakamilika, hivyo kuomba tarehe nyingine ya kusikiliza huku akisema katika taarifa ya awali Msemwa alijichanganya kuitaka mahakama iwape dhamana watuhumiwa wakati sheria zipo wazi kwamba makosa hayo hayana dhamana.
ONYO KALI
Hakimu Mashauri alikubali ombi la upande wa mashtka la kuwaonya Mawakili waakina Malinzi kuacha tabia ya kutumia vyombo vya habari na kwamba wafuate taratibu za kisheria ikiwemo kukata rufaa Mahakama Kuu pale wanapoona hawatendewi haki.
“Sheria iko wazi, upelelezi haujakamilika, si busara kwenda kulalamika kwenye vyombo vya habari, naomba hilo liachwe mara moja na hamzuiwi kuzungumza na vyombo vya habari ila kwa kufuata misingi na taratibu na si kupotosha umma, kama inashindikana basi muwalete mawakili wengine wanaojua kufuata taratibu za kimahakama,” alisema Mashauri.     

Related

michezo na burudani 5361354926500360348

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii