Waziri mkuu kawapa neno makatibu wakuu

Makatibu wakuu wa wizara za Nishati na Madini; Fedha na Mipango; na Ujenzi na Uchukuzi wamebebeshwa jukumu la kuangalia namna ya kuondoa vikwazo vya utekelezaji wa katika ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Kinyerezi. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo jana alipotembelea mradi huo wa kufua umeme kwa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi II ambao ukikamilika, utatoa umeme wa Megawati 240 katika Gridi ya Taifa. Miongoni mwa vikwazo katika utekelezaji wa mradi huo ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika mitambo na gharama za uendeshaji. Hata hivyo, Majaliwa amesema changamoto hizo zote zipo ndani ya Serikali kuanzia tozo za VAT katika uingizaji wa mitambo, gharama za uendeshaji sanjari na tozo za usafishaji wa mizigo zilizowekwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads). “Ukiona kuna shida ya tozo VAT kwa ajili ya mitambo vifaa, katibu mkuu (Nishati na Madini) zungumza na katibu mkuu wa Wizara ya Fedha. Tunachotaka miradi yetu isikwame. “Kama mnadhani Tanroads inakwaza kwa tozo zake na kusababisha gharama kubwa hadi ya mradi, nenda zungumza na katibu mkuu wa uchukuzi ili muone mtakavyowezesha ili miradi hii ikamilike,” amesema Majaliwa. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amesema mradi huo unapita katika hatua mbalimbali kuanzia namba moja hadi nne. “Mradi wa Kinyerezi namba moja umeshakamilika na kwa sasa tupo namba mbili ambao ujenzi wake ulianza Machi mwaka jana. Baadaye tutakwenda namba tatu na nne,” amesema Profesa Mdoe.

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii