Madini ya kutengeneza vifaa vya simu kuchakatwa nchini



Mtambo wa kwanza barani Afrika kwa ajili ya kuchakata madini ghafi ya tantalum na niobium wenye thamani ya Dola 40 milioni utaanzishwa nchini mwakani.
Madini hayo hutumika kutengeneza vifaa kama vile simu, kompyuta, injini za ndege, betri za magari na vifaa vya umeme.
Mtambo huo unaotumia mashine zenye teknolojia ya hali ya juu ni za kampuni ya kimataifa ya AB Minerals ya nchini Canada ukilenga kuongeza thamani ya madini hayo.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Frank Balestra leo Jumatatu amelieleza Mwananchi kuwa mitambo hiyo ni rafiki kwa mazingira kwa kuwa inatumia umeme mdogo na uendeshaji wake ni wa gharama nafuu.
Amesema mitambo hiyo itasimamiwa na kuendeshwa na Kituo cha Madini Afrika (AMGC) ambacho kimekuwa kikifanya uchenjuaji, utafiti na utathmini wa madini.
Balestra amesema mitambo hiyo ina uwezo wa kuchakata tani 3,000 za madini ghafi kwa mwaka na itasaidia kupata thamani halisi ya madini na kuyauza kwa bei ya juu.
"Ni mfumo wa kwanza Afrika, tunataka kusaidia sekta ya madini na kufanya wachimbaji wauze madini moja kwa moja kwenye soko," amesema
Balestra amesema, "Kuna umeme wa kutosha na mazingira ni rafiki hapa. Pia, Kituo cha Madini kina watu wenye ujuzi mkubwa na maabara zao ni za kisasa, hii itaongeza kasi ya uzalishaji."
Amesema anaamini huu ni wakati muafaka wa kuleta teknolojia hiyo kwa kuwa Serikali ya Tanzania inahimiza kulinda rasilimali na hasa madini. Mitambo hiyo amesema inatarajiwa kuanza uzalishaji Septemba mwakani.

Related

uchumi na biashara 8638557868758851306

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii