De Bruyne: Mo Salah mchezaji bora England

http://maisharaisi.blogspot.com/2018/04/de-bruyne-mo-salah-mchezaji-bora-england.html

Kevin de Bruyne amesema kuwa yeye ni namba moja, lakini Mohamed Salah wa Liverpool ndiye mchezaji bora wa Lig Kuu England msimu huu.
De Bruyne na Salah wameingia katika orodha ya wachezaji wanapewa nafasi ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora msimu huu, baada ya kucheza kwa kiwango bora.
Wakati De Bruyne, nyota wa kimataifa wa Ubelgiji amekuwa chachu ya mafanikio Manchester City, mabao ya Salah yanamuweka katika rekodi nzuri msimu huu.
De Bruyne ana amini Salah amekuwa kwenye kiwango bora zaidi yake na ana nafasi kubwa ya kumpiku katika tuzo ya mwaka huu.
Nyota wanatarajiwa kukutana uso kwa uso leo katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao Liverpool itakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Anfield kuikaribisha Man City.
“Sawa, kama nitapata mimi itakuwa jambo jema kwangu na klabu. Binafsi najiona niko kwenye kiwango bora nimecheza kwa ufanisi zaidi. Kwa upande mmoja naamini nistahili,” alisema De Bruyne.
Mchezaji huyo alimtaja Salah ni mshambuliaji mwenye kiwango bora msimu huu na mabao yake yamekuwa chachu ya mafanikio katika kikosi cha Liverpool.