Ripoti wawekezaji viwanda vya dawa kupelekwa kwa mawaziri





Wakati ripoti ya wawekezaji wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa nchini ikitarajiwa kufikishwa katika Baraza la Mawaziri wiki hii, imebainika kuwa zaidi ya wawekezaji 30 waliojitokeza wana ujuzi, ardhi na mawazo lakini hawana mitaji.
Wawekezaji 38 walipatikana baada ya kikao cha Aprili 4 kati ya wafanyabishara hao na Serikali, huku Aprili 5 kikifanyika kikao cha ndani baina yao na wengine 30 wenye ujuzi waliojitokeza.
Suala hilo limekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kukaribisha wawekezaji kujenga viwanda vya dawa kukabiliana na upungufu uliopo katika sekta hiyo, wakati akizindua magari 181 ya Bohari ya Dawa (MSD), Machi 26.
Akizungumza  juzi, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema kwa sasa wizara yake na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji zimekamilisha kazi ya awali na kuandaa ripoti itakayopelekwa Baraza la Mawaziri.
Naye mkurugenzi mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema ili kufikia hitaji la dawa wamekuwa wakiingiza kati ya asilimia 85 hadi 94 ya dawa zote na vifaatiba vinavyohitajika kutoka mataifa ya nje, hivyo zaidi ya Dola 500 milioni za Marekani zikitumika.

Related

kimataifa 1233522296182404879

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii