Mrisho Gambo msibani kwa Leyla Mtumwa




 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anatarajiwa kuongoza mamia ya waombolezaji katika  mazishi ya Mtanzania, Leyla Mtumwa aliyeuawa Uingereza.
Leyla anadaiwa kuchomwa visu hadi kufa Machi 30 mwaka huu na mume wake, Kema Kasambula, nyumbani kwa wanandoa hao, Kirkstall Avenue, Haringey, Uingereza.
Mwili wa Leyla, uliwasili jana ukitokea Uingereza na anatarajiwa kuzikwa leo jioni mjini hapo.
Kwa sasa, kisomo cha hitma kinaendelea nyumbani kwao, eneo la Kaloleni, Arusha.

Related

blog 1300046051375902688

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii