Taratibu za kuurejesha mwili wa aliyeuawa London zaendelea
 
http://maisharaisi.blogspot.com/2018/04/taratibu-za-kuurejesha-mwili-wa.html
 Taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa tayari kitengo cha polisi cha uchunguzi wa mauaji hayo, kimeshakamilisha uchunguzi wao na sasa zinasubiriwa taratibu nyingine za kuruhusu mwili huo kurejeshwa nchini.
“Michango inaendelea vizuri, kila kitu kipo sawa, uhakika wa kumrudisha Tanzania upo, lakini bado taratibu ndogo ndogo tu, na tutawajuza.” Kimesema  chanzo kimoja kutoka nchini humo.
Leyla, anadaiwa kuchomwa visu hadi kufa  na mumewe, usiku wa kuamkia Machi 29 huko eneo la Tottenham, Uingereza.
Leyla ni mtoto wa Hidaya Mtumwa, mwanamke aliyewahi kutungiwa wimbo na mwanamuziki Pepe Kalee, miaka 1990.

