Mbunge Mlinga ampa meno IGP




Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kutumia nguvu alizonazo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwatukana viongozi.
Akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya ndani kwa 2018/19, Mlinga amesema; “Matusi mitandaoni yamejaa, hajulikani Rais ni nani, kiongozi ni nani, kuna akaunti nyingi zinatukana, IGP (Sirro) tumekuwekea nyota mabegani tumia nguvu zako.”
Mlinga licha ya kupongeza utendaji wa polisi, amedai asilimia 85 ya huduma inayotolewa na jeshi hilo inahusisha rushwa ingawa anasema askari wa kike hawamo kwenye kundi hilo.
“Kesi ya kuku inakuwa ya ng’ombe, kesi ya kutusi inakuwa ya kuua kwa maneno, lakini niwapongeze wanawake katika hili hawamo,” amesema Mlinga huku akishangiliwa.
Amesema matukio ya kamatakamata yanayofanywa na Trafiki: “Ni janga la Taifa, wanaitwa wana mapato Dar es Salaam huko wanaitwa Tigo. Bodaboda ndiyo kabisa usiseme, ukienda katika vituo vya polisi, pikipiki ni nyingi.”
Naye mbunge wa Mlimba (Chadema), Susan Kiwanga amesema; “Kazi ya polisi si kunipangia cha kusema katika mkutano. Kama unaona nakosea subiri niongee nikimaliza  ukiona nimekosea nikamate.”

Related

kitaifa 2261558991347025643

Post a Comment

emo-but-icon

item
Kicbjamii