Rais JPM awaapisha mawaziri wapya
 
http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/rais-jpm-awaapisha-mawaziri-wapya.html

Rais Magufuli 
 Rais John Magufuli amewaapisha mawaziri wawili aliowateua hivi karibuni  katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali.
Mawaziri walioapishwa leo ni Profesa Palamagamba Kabudi,aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Sheria na Katiba na Harrison Mwakyembe aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Profesa Kabudi anaenda kuongoza wizara iliyokuwa ikiongozwa na Dk Mwakyembe
Wakati Mwakyembe anashika nafasi ya Nape Nnauye aliyebadilishwa  hivi karibuni.
