Yanga yatozwa fain

http://maisharaisi.blogspot.com/2017/03/yanga-yatozwa-fain.html
Kamati ya Bodi ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Tanzania (Kamati ya Saa 72), imeipiga Yanga faini ya Sh500,000 kwa kutumia mlango usio rasmi kuingia Uwanjani. Kamati hiyo iliyokutana mwishoni mwa wiki ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom ikiwamo mechi kati ya Simba na Yanga iliyochezwa Februari 25, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa. Katika mchezo huo Yanga iliingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.